Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) imeendelea kuimarisha uhusiano na wateja wake kupitia maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, yanayofanyika kitaifa kuanzia tarehe 6 hadi 11 Oktoba 2025, kwa kaulimbiu isemayo Huduma Bora za TVLA ni Haki ya kila mteja kuadhimisha wiki hiyo, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TVLA, Bw. Furaha Kabuje, alifanya ziara maalum katika baadhi ya maduka yanayouza bidhaa za TVLA jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2025 kwa lengo la kusikiliza maoni ya wadau mbalimbali hususan wauzaji wa bidhaa na wanufaika na huduma zinazotolewa na Wakala.
Saturday 1 November 2025
⁞
